MCHEZAJI KAHUKUMIWA MIEZI 6 JELA KWA KUDANGANYA UMRI
Taarifa ya kijana Gouray Mukhi kutokea India imekuwa gumzo mitandaoni kote kufuatia kukumbana na adhabu ya kifungo cha miezi 6 jela kutokana na kufanya udanganyifu wa umri wake katika mchezo wa soka na kutambulika kama mchezaji mwenye umri wamiaka 16 tofauti na umri wake halisi.
Gouray Mukhi ambaye amedanganya umri wake kwa kushusha kutoka umri wa miaka 28 ambao ndio umri wake sahihi na kushusha hadi umri wa miaka 16, amehukumiwa jela miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa hilo la unganyifu wa umri ambao kwa kawaida unahusisha na kufoji nyaraka za hati ya kuzaliwa.
Hata hivyo uongo huo ambao ulimfanya Gouray Mukhi atambulike kama ndio mchezaji wenye umri mdogo zaidi kufuga goli katika michuano ya Ligi Kuu nchini India October 7 wakati huo wa kimtambua kama mchezaji mwenye umri wa miaka 16 na sio 28 kama ambavyo imethibitika