ZAHERA KAONDOKA TANZANIA ILA KAWATOA HOFU MASHABIKI WA YANGA
Baada ya vuta nikuvute na stori za hapa na pale kuhusiana na kocha mkuu wa Yanga mwenye uraia wa Congo na Ufaransa Mwinyi Zahera kutaka kuachana na timu hiyo kwa madai yauwepo wa mambo ya ovyo kutoka kwa viongozi, leo alitoa taharuki baada yakuonekana uwanja wa ndege akitaka kuondoka.
Mwinyi Zahera baada ya mchezo wa Yanga dhidi ya Ruvu Shooting uliyomalizika kwa Yanga kupata ushindi wa mabao 3-2, aliweka wazi kuwa alitaka kuacha timu hivyo kutokana na uongozi kufanya usajili pasipo na mapendekezo yake hivyo alitaka kuachana na timu hiyo ila mapenzi yake kwa mashabiki ndio yalimfanya aendelee na timu hiyo.
Mwalimu Zahera alishituka kusikia kuwa meneja wa timu yao Afizi anamwambia kuwa uongozi umemsajili mlinda mlango mpya, kitu ambacho hakikuafikia na hakumkubali mchezaji huyo na kusema yeye alipendekeza Boban na wachezaji wengine ambao hawakusajiliwa.
Baada yakuonekana uwanja wa ndege Zahera akahisiwa kaamua kusepa ndipo alipoweka wazi kwa kusema anaenda Ufaransa kwa muda kushughulikia mambo yake ila anarudi tarehe 26 siku ya Boxing Day kuendelea na kazi kama kawaida.
“Nasafiri leo narudi tarehe 26 nitaondoka Ufaransa tarehe 25 naenda kwa sababu kuna makaratasi ya kusaini makaratasi ya nyumbani kutokana na mambo yangu ya biashara ya Ulaya, tarehe 26 asubuhi narudi, watu wanaosema kocha anaenda uongo mimi mwenyewe navumilia wachezaji wangu kuvumilia na matatizo ndio mimi leo niondoke kwa sababu ya matatizo ni uongo”alisema Mwinyi Zahera
Pamoja na kudaiwa kuwa katika hali mbaya ya kiuchumi Yanga wanaongoza Ligi kwa kuwa na jumla ya alama 44 walizovuna katika michezo 16, wakishinda michezo 14 na sare michezo miwili wakiendelea kubakia klabu pekee wao na Azam FC kuwa ndio hawajaruhusu kupoteza mchezo, Azam FC wakiwa nafasi ya pili kuwa na alama 40 wakicheza michezo 16 sawa na Yanga.