Safari ya Kahata kwenda Algeria yagonga mwamba
Kiungo wa Gor Mahia Francis Kahata huenda asijiunge na klabu ya Algeria, CS Constaine baada ya mazungumzo kugonga mwamba.
Kahata ambaye ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Kenya alikuwa anatarajiwa kuelekea Algeria baada ya klabu hiyo ya daraja ya kwanza kuonyesha nia.
Kulingana na tetesi kutoka Algeria, kiungo huyo huenda asijiunge na timu hiyo baada ya mazungumzo kutibuka.
“Walishindwa kuafikiana na kwa sasa Kahata atasalia Gor Mahia. Mchezaji alikuwa anataka kujiunga nao lakini wakakosa kuafikiana,” alidokeza msimamizi mmoja wa Gor Mahia.
Kahata alichezea Gor Mahia dhidi ya Lobi Stars ya Nigeria siku ya Jumapili katika kombe la Klabu Bingwa Afrika ambapo Gor Mahia iliondoka na ushindi wa 3-1