Kikosi cha Simba kurejea saa 9 usiku
Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea nyumbani Tanzania leo saa 9:40 usiku kikitokea nchini Zambia, ambapo hapo jana kilikuwa na mchezo wa kwanza dhidi ya Nkana kwenye kombe la klabu bingwa Afrika; Nkana 2 – 1 Simba SC
Kupitia ukurasa wa Instagram wa klabu ya Simba, imetoa taarifa rasmi kuhusiana na kurejea kwa kikosi cha Simba ambapo kiliwasili Uwanja wa ndege wa Ndola, Zambia saa 7:04 mchana tayari kuanza safari kurejea Tanzania.